Waweka nguvu upandaji miti

KATAVI; Tanganyika. Halmashauri ya Wilaya Tanganyika Mkoa wa Katavi, leo imeanza maadhimisho ya siku ya Uhuru kwa kupanda miti 1000 katika Kijiji cha Majalilla.

Tukio hilo limeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu akiambatana na viongozi mbalimbali wa halmashauri hiyo, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wataalamu na wananchi wa Kijiji cha Majalila.

Advertisement

Akizungumza DC Buswelu amemataka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika kupitia wataalamu wake kushirikiana na wananchi wa Kijiji cha Majalila kutunza miti hiyo kwa manufaa ya kizazi kijacho.

Pia kutokana na miti hiyo kupandwa kando mwa barabara kuu iendayo Kigoma, amemwagiza Katibu Tawala wa wilaya ya hiyo kumwandikia barua Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Katavi ashirikiane na viongozi wa kijiji, ili kuitunza miti hiyo kwa pamoja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Hamad Mapengo amesema upandaji miti katika Wilaya ya Tanganyika ni endelevu na kwa sasa wataendelea ngazi ya kata na vijiji.

1 comments

Comments are closed.

/* */