Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amewatembelea wahanga wa maafa walioezuliwa na kubomolewa makazi yao katika kata ya Kizumbi na Mwamala kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia Novemba 6, 2023.
Mndeme alisema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Samia Suluhu Hassan imepokea masikitiko makubwa taatifa za mafuriko haya na kwamba itatia huduma ya matibabu bure mpaka kupona kwa majeruhi wote, italeta mbegu kwa wathirika wa mashamba, italeta vifaa vya kulalia na itafanya tathimini ya awali ili kujuwa kiasi cha hasara iliyopatikqna na mahitaji halisi.
“Poleni ndugu zetu kwa tukio hili, lakini niseme kuwa serkali itagharamia matibabu wa majeruhi, kuleta mbegu, vifaa vya kulalia, pia nimuagize Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga kufanya tathimini ya awali kujuwa uhalisia wa mahitaji na hasara iliyopatikana ili serikali ijue ichukue hatua alisema Mhe. Mndeme.
Diwani wa Kata ya Kizumbi Reuben Kitinya alisema mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia tarehe 6 Novemba, 2023 iliyoambatana na upepo mkali pamoja na barafu ndiyo iliyoleta athari yote hiyo huku akisema jumla ya nyumba 31 zimeathirika kwa kung’olewa bati na kaya 27 kubomoka kabisa.
Kwenye kata ya Mwamala jumla ya nyumba 51 zimeathirika na mvua hizo pamoja na hekari takribani 10 kuharibiwa kabisa na mvua ya barafu iliyoambatana na upepo mkali katika kijiji cha Ng’onze na kuumiza watu wanne akiwemo bibi kizee ambaye amelazwa hospitali ya Mwawaza.
Mndeme alitoa wito kwa wananchi wote kuendelea kuchukua tahadhari ya mvua hizi zilizotabiriwa na Mamlaka ya hali ya hewa kuwa zitakuwa za juu ya kiwango, kuondoka maeneo yote hatarishi.