WATU 47 wamefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kukutwa na Bangi kilo 82 kinyume cha Sheria, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara Nicodemus Katembo amesema wakati akitoa taarifa waandishi wa habari.
Tukio hilo limetokea kufuatia msako uliofanywa na Askari wa Jeshi la Polisi katika kipindi cha Septemba na Oktoba mwaka huu.
“Katika kipindi hiki cha miezi miwili Septemba na Oktoba mwaka huu Askali wa Jeshi hilo limefanikiwa kukamata Watuhumiwa wa makosa mbalimbali ikiwemo Bangi kilo 82 na gramu 564 na Watuhumiwa hao wote wamefikishwa Mahakamani,” amesema.