Ucheleweshwaji mizigo bandarini kupatiwa ufumbuzi

CHANGAMOTO  ya uchelewashwaji wa mizigo bandarini huenda ikapatiwa ufumbuzi.

Hayo yamethibitishwa leo Februari 08, 2024, jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge la Afrika Mashariki, Francine Rutazana kamati inayohusika na uwezeshaji wa kufanyika kwa biashara Afrika Mashariki, wakati kamati hiyo ilipofanya ziara katika bandari ya Dar es Salaam kuona namna uendeshaji na uhudumiaji wa bandari inavyoendeshwa na kuhudumia nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

Rutazana amesema baada ya maongezi na maofisa wateja , waendeshaji wa bandari na wadau mbalimbali wamethibitisha kupokea huduma nzuri kutoka katika Bandari Dar es Salaam huku akieeleza kuwa kuna changamoto ya ucheleweshaji wa upakuaji wa mizigo kwenda kwa wateja wake wa nchi uanachama wa jumuiya hiyo.

Advertisement

“Tumekutana na waendeshaji wa bandari kujua ni namna gani tunaweza kuimairisha changamoto ya ucheleweshaji wa mizigo ambayo baada ya ukakuguzi huu tunajukumu la kuandika ripoti kwa Baraza la Mawaziri lenye jukumu la kusimamia mapendekezo ya bunge hili, na hivyo tunatoa muda ambao kama mapendekezo hayo hayatafanyiwa kazi tunajukumu la kufuatilia mpaka pale yatakapofanyiwa kazi na biashara ikaendelea kufanyika kama kamati inavyotaka”. Rutanzana amesema.

Hata hivyo kamati hiyo inajukumu la kuunda sheria itakayo wezesha ufanyikaji wa biashara katika jumuiya hiyo.

Mjumbe wa bunge hilo na mwakilishi kutoka Kenya, David Ole Sankok, amesema kuwa wameridhishwa na namna bandari ya Tanzania inavyohudumia jumuiya hiyo, huku akiishauri Tanzania kutafuta wataalamu wa uchumi wa bluu ili waweze kuwekeza kwenye uchumi wa bluu kutokana na nafasi kubwa waliyonayo ya uwepo wa maziwa makubwa, akiishauri kujenga bandari itakayo sambaza bidhaa kutoka Ulaya, Mashariki ya mbali na Marekani kwenda kwenye nchi nyingine za Afrika.

Kwa upande wake Mussa Biboze, aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, amesema kuwa kwasasa wanaendelea kujipanga kuhudumia Meli kubwa na kuandaa maeneo maalumu mapya ambayo yako tayari kwaajili ya upokeaji wa mizogo hiyo ili kurahisisha na kufaifanya bandari isiwe na msongamano, ambapo maeneo hayo yaliyopo nje ya bandari yatatumika kotolea mizigo nje ya bandari.