Serikali kupunguza uhaba watumishi wa afya

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema miongoni mwa vipaumbele vya Serikali ni kuajiri watumishi wa afya ili kupunguza changamoto za uhaba wa watumishi wanaoweza kutoa huduma za afya kwa Watanzania.

Ummy amesema hayo leo Februari 12, 2024 bungeni wakati akichangia taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kamati kwa mwaka 2023 katika Bunge la 12, mkutano wa 14 kikao cha 10 jijini Dodoma.

“Serikali tunaendelea kutumia fedha za wadau kuajiri wataalamu wa Afya wa mikataba, lakini pia tulizindua wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii ili kuwapunguzia mzigo wa watumishi wa Afya katika vituo vya kutoa huduma za Afya”. amesema Ummy.

Wakati huo huo Waziri Ummy amesema wizara hiyo inafuata miongozo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ambayo inasema afya ni ukamilifu wa binadamu kimwili, kiakili, kijamii na kutokuwepo kwa magonjwa ambapo sera hiyo inataka huduma itolewe kwa kuzingatia mahitaji ya kila mtu.

Habari Zifananazo

Back to top button