Nondo amtaja mgombea mwenza ngome ya vijana

MWENYEKITI Ngome ya Vijana ya chama cha ACT Wazalendo amemtangaza Nassor Ahmed Marhun kuwa mgombea mwenza wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana katika uchaguzi utakaofanyika Februari 29, 2024.

Nondo ametoa taarifa hiyo leo Februari 16, 2024 kupitia mitandao yake ya kijamii ambapo amesema mwenza huyo ni kutoka tawi la Utaani-Wete, Pemba Zanzibar.

Katika taarifa hiyo Nondo ameandika: “Napenda kumtangaza rasmi ndugu, Nassor Ahmed Marhun mwanachama na kijana mwenzangu kuwa mgombea mwenza wa nafasi hii ya uenyekiti wa Ngome ya Vijana Taifa”.

Februari 5, 2024 kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Nondo alitoa taarifa ya kugombea kwa mara nyingine nafasi ya uenyekiti wa ngome hiyo, ambapo pia aliwataka vijana wenzake wa chama hicho kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali.

Habari Zifananazo

Back to top button