Vitambulisho vya machinga kurudi – Chalamila

DAR ES SALAAM, Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila, ametoa tangazo la kurudishwa kwa vitambulisho vya biashara kwa wafanyabiashara wadogo.

Hatua hii imechukuliwa kufuatia kilio kirefu cha wafanyabiashara hao, ambapo Rais Samia anapanga kurejesha vitambulisho hivyo kwa gharama ile ile kama ilivyokuwa wakati wa utawala wa Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt. John Magufuli.

Advertisement

Chalamila ametoa kauli hiyo leo Februari 28,2024 wakati wa kutoa ripoti ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Mkoa wa Dar es Salaam, katika kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abbasi Mtemvu.