Kinana: ‘Dhamira ya Rais uchaguzi kuwa huru na haki’

DAR ES SALAM: Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amesema dhamira ya kweli ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuachia uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani kuwa huru na haki.

Kinana ameyasema hayo leo Machi 5, 2024 katika Ufunguzi wa Mkutano wa Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo unaoendelea kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

“Tunakwenda uchaguzi wa serikali za Mitaa, na mwakani uchaguzi mkuu mabadiliko matatu ya sheria yamefanyika, sheria ya uchaguzi, tume ya uchaguzi, vyama vya siasa,”amesema Kinana na kuongeza:

“Serikali ya CCM chini ya Mwenyekiti wake Rais Samia Suluhu Hassan ina dhamira ya dhati mwaka huu uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu kuhakikisha kunakuwa na uchaguzi huru na wa haki.

Aidha, amesema maoni mbali mbali yaliyotolewa kwenye Kamati za Bunge, kumefanyika mabadiliko makubwa, serikali ya CCM ina dhamira ya dhati mwaka huu wa uchaguzi wa serikali za Mitaa, uchaguzi Mkuu kuhakikisha una kuwa uchaguzi huru na wa haki.

“Kuna sheria na dhamira unaweza kuwa na sheria nzuri kama huna dhamira nzuri unaweza kuikanyaga ile sheria na kufanya unavyotaka.

“Unaweza kuwa na dhamira nzuri na sheria mbaya, dhamira ikitawala mambo yatakuwa mazuri;….. “Rais ameamua kwamba uchaguzi mwaka huu na ujao utakuwa huru na wa haki.

“Nahakika wapo ambao wana mashaka na kauli hii, na hao wenye mashaka wanazo sababu na sababu zao zinatokana na uchaguzi wa mwaka 2019 na ule wa mwaka 2020 huo ndio ukweli.

“Sheria tuliyokuwa nao kwenye uchaguzi iliyotupeleka uchaguzi 2015 iliwezesha wanachama 117 kuingia bungeni, asilimia 40 ya madiwani kuiniga kwenye nafasi za halmashauri.

“Mwaka 2020, msema kweli mpenzi wa Mungu lazima tuseme ukweli, hofu ya watanzania na ya wenzangu vyama vya siasa, hasasi za kiraia, baadhi ya viongozi wa dini ni yale yaliyotokea 2019,2020, niwahakikishie Rais Samia Suluhu Hassan ameamua uchaguzi utaachiwa wapiga kura uamuzi wao ndio utoe tafsiri ya uchaguzi.

“Hata wabunge kukubali kufanya marekebisho ni kwa sababu ya dhamira ya viongozi wa taifa letu, nimewahi kusema huko nyuma na narudia tena hakuna muswada uliopewa muda mrefu kusikiliza wadau kama hii ilipewa siku nne ilikuwa ijadiliwe siku moja kwa umuhimu wake ulijadiliwa siku nne.

“Marekebisho mengi sana yamefanyika na Rais karidhia yeye asiteuwe Mwenyekiti na Makamu na badala yake wapendekezewe,”amesema Kinana

Amesema, leo kuna sheria bora zaidi ya sheria yam waka 2015 ambayo iliingiza madarakana wabunge wa upinzania 117 na asilimia 40 ya madiwani kwenye halmashauri.

“Nasisitiza hivi kwa sababu nataka muamini dhamira ya njema ya Rais Samia na serikali yake.” Amesisitiza.

Habari Zifananazo

Back to top button