Jude afungiwa mechi mbili

KIUNGO wa Real Madrid, Jude Bellingham amefungiwa michezo miwili ya La Liga baada ya kumfanyia vurugu mwamuzi katika mchezo ulioisha sare ya 2-2 dhidi ya Valencia wiki iliyopita.

Bellingham, 20, alidhani alifunga bao la ushindi dakika sita baada ya dakika za lala salama wakati huo mwamuzi alishapuliza filimbi kuashiria kumalizika kwa mchezo.

Video za marejeo zilionesha mwamuzi Gil Manzano alipuliza filimbi wakati krosi inapigwa, kabla ya Jude kufunga bao hilo.

Advertisement

Shirikisho la Soka la Uhispania (RFEF) lilisema Bellingham alionyesha “dharau au kutomjali” Manzano wakati wachezaji na wafanyikazi wa Madrid walipomzunguka wakitaka bao hilo likubaliwe.

Bellingham, ambaye alikuwa akirejea baada ya wiki tatu nje ya uwanja kutokana na jeraha la kifundo cha mguu, alipigwa faini ya Euro 600.

Real ilikata rufaa dhidi ya kadi nyekundu ya Bellingham lakini kamati ya nidhamu ya RFEF ilitupilia mbali hoja yao kwamba mwamuzi alifanya kosa.