MSHAMBULIAJI Prince Dube ametangaza kuachana na Azam FC baada ya kudumu klabuni hapo kwa miaka minne.
Awali kulikuwa na taarifa za Mzimbabwe huyo kuomba kuondoka ,Azam FC walithibitisha taarifa hizo na kuweka wazi kuwa hawamzuii ila taratibu zifuatwe.
Katika mchezo wa jana dhidi ya Coastal Union, Dube hakuwa sehemu ya kikosi.
Dube ametangaza kuachana na timu hiyo leo kupitia mitandao ya kijamii.