Bugando kuanza upandikizaji figo

HOSPITALI ya Rufaa ya Kanda Bugando, mkoani Mwanza itaanza kutoa huduma za upandikizaji figo mwishoni mwa mwaka huu.

Hatua hiyo ni kufuatia ongezeko la wagonjwa wa figo, ambapo hospitali hiyo inahudumia wagonjwa wapya kati ya 15 hadi 20 kwa siku, kutoka wanne kwa siku wakati Bugando inaanzisha matibabu ya figo, miaka ya 1970.

Daktari bingwa bobezi wa figo Bugando, Said Kanenda amesema leo katika maadhimisho ya siku ya figo duniani kwamba huduma za upandikizaji figo ndiyo tiba ya uhakika zaidi.

Advertisement

“Kwa sasa tunatoa huduma ya kusafisha figo tu na tunashukuru serikali kuendelea kufanya maboresho sekta ya afya kwasababu hadi sasa tuna mashine takribani 27 za usafishaji,”

“Na sasa serikali inaelekea kuwezesha utoaji huduma ya uhakika kwa kupandikiza figo, ambayo itamuwezesha mgonjwa kurudi hali yake ya zamani,” amesema.