RC Mtwara akabidhiwa ofisi

MAKABIDHIANO ya Ofisi kati ya Mkuu wa Mkoa mpya wa Mtwara na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Kanali Ahmed Abbas yamefanyika leo mkoani humo.

Hatua hiyo imekuja kufuatia mabadiliko ya uteuzi yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa viongozi katika maeneo mbalimbali nchini Machi 9, 2024.

Aidha anayekabidhi ofisi hiyo ni Kanali Ahmed Abbas aliyehamishiwa kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na anayekabidhiwa ni Kanali Patrick Sawala aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba mkoani humo.

Akizungumza katika ghafla hiyo, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee mkoani humo Meja Mstaafu Mohamedi Mbwana amewaomba viongozi hao kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha anatekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na jamii.

“Muepuke makundi yanayoleta mfarakano na kukosekana kwa umoja, kwahiyo kitu kikubwa ni mshikamano ili muweze kufanya kazi vizuri hayo ndio maneno yangu”amesema Mbwana

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara Saidi Nyengedi amesema ni matumaini yake makubwa kuwa yale yaliyofanywa na mkuu huyo anayeondoka yataendelezwa na anayekuja kwasababu wote walikuwa wakifanya kazi pamoja.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Ruvuma, amesema moja ya sifa ya kiongozi ni kuweka wazi milango ili kupata ya watu kuja kuwasilisha hoja zao na kuzifanyia kazi.

Hata hiyo amemshukuru,kumpongeza Rais Dk Samia kwa kumuamini na kuendelea kumuweka katika nafasi ya uongozi.

Aidha, amesisitiza suala hilo la kuepuka makundi  kwa Mkuu huyo wa mkoa mpya ili aweze kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa.

‘Kikubwa ni kuacha milango wazi ili kusikiliza hoja ya kila mtu na kusimamia haki kwa makundi yote”amesema Abbas

Mkuu huyo wa mkoa mpya, ameomba ridhaa kwa wanamtwara huhusu yeye kuja kushika nafasi hiyo kwenye mkoa huo.

Aidha amesisitiza saula la  mshikamano baina ya viongozi na jamii hiyo ili waweze kuendeleza yale yaliyofanywa na mkuu wa mkoa aliyeondoka.

Habari Zifananazo

Back to top button