‘Aprili 10 ni Eid al Fitri’

DAR ES SALAAM: MUFTI Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally amethibitisha mwandamo wa mwezi wa Shawwal.
Akitoa taarifa hiyo kwa wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Mufti Zubeir amekiri kupokea taarifa za mwandamo kutoka kwa Mufti Mkuu wa Zanzibar pia kutoka nchi jirani ya Kenya.
“Kesho Aprili 10, 2024 itakuwa ni Eid al Fitri, hivyo nawatakia Eid njema,” amesema kiongozi huyo.
Eid al Fitri ni Sikukuu inayoadhimishwa kila mwaka na Waumini wa Dini ya Kiislamu baada ya kutamati kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Habari Zifananazo

Back to top button