Vijana wajengewa mazingira fursa za ajira

DAR ES SALAAM: OFISI ya Waziri Mkuu,kazi ,Vijana, Ajira na wenye ulemavu imeanzisha programu maalumu za kukuza ujuzi kwa vijana yenye lengo la kuwapatia ajira na fursa mbalimbali

Hayo amesema Yohana Madadi, Mkurugenzi Mkuzaji Tija, Ofisi ya Waziri Mkuu  kwenye kongamano lililoandiliwa na Taasisi ya Leberity Sparks lililowakutanisha zaidi ya wanafunzi 300 kutoka vyuo mbalimbali nchini.

Advertisement

Pia amewaeleza washiriki kuwa kuna mfuko unaojulikana kama  3.3.2 kila Halmashauri nchini, ambao unakopesha vijana na kuwapa fursa kushiriki maendeleo ya nchi

Amesema kongamano hilo litasaidia vijana kujadili mawazo mapya na kuleta uvumbuzi pamoja na ubunifu katika suala la maendeleo yao, huku akitoa wito kwa vijana wanatakiwa wathubutu na wawe wajasiri kufanya maendeleo.

Naye Mkurugenzi wa wa Leberty Sparks,  Evance Exaud amesema kongamano hilo litaleta muamko wa vijana kwenye maendeleo kwa kuweka ubunufu utakaosaidia jamii katika ukuaji wa uchumi.