660 wafariki kipindupindu-WHO

#KIMATAIFA: Shirika la Afya Duniani (WHO) limeeleza kuwa vifo 660 na wagonjwa 26,000 wameripotiwa hadi kufikia Januari 29, 2023 katika nchi kumi za Afrika zinazokabiliwa na mlipuko wa ugonwa wa Kipundupindu.

Kwa mujibu wa Ofisi ya WHO kanda ya Afrika, iliyopo Brazzaville, nchini DR Congo wagonjwa 80,000 na vifo 1,863 vimerikodiwa katika nchi 15 zilizoathirika katika mwaka 2022, huku wagonjwa 141,467 na vifo 4,094 vikiripotiwa mwaka 2021.

WHO imeonya ongezeko kubwa la wagonjwa wa kipindupindu kufuatia wimbi kubwa la ugonjwa huo duniani, ambapo idadi ya wagonjwa waliorikodiwa barani humo katika mwezi wa kwanza mwaka 2023 pekee imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 30 ya idadi ya jumla ya mwaka mzima wa 2022.

Advertisement

Imeelezwa kuwa kama wimbi hili la ugonjwa litaendelea kuongezeka kwa kasi maambukizi katika mwaka huu yanaweza kupita idadi ya wagonjwa iliyorikodiwa mwaka 2021.

Wastani wa idadi ya vifo kwa hivi sasa ni karibu asilimia 3, ambayo imepita asilimia 2.3 ya mwaka 2022, huku kiwango kinachokubalika cha ongezeko ni chini ya asilimia 1.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *