Bola Tinubu aapishwa kuwa Rais wa Nigeria

Bola Tinubu ameapishwa kuwa rais wa tano wa Nigeria.

Tinubu amekula kiapo katika ka katika uwanja wa Eagle Square mjini Abuja na kushangiliwa na umati wa watu.

Mkewe, Oluremi Tinubu, alisimama kando yake alipokuwa akila kiapo chake na kutia sahihi nyaraka.

Rais Tinubu atalazimika kukabiliana na uchumi unaosuasua na ukosefu wa usalama ulioenea katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika.

Kashim Shettima pia ameapishwa kama makamu wa rais mpya wa Nigeria katika hafla hiyo.

Hafla ya kuapishwa kwa Tinubu imesimamiwa na maafisa wa mahakama alipokuwa akila kiapo na kutia saini nyaraka.

Hafla ya hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Afrika akiwemo Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,  Paul Kagame wa Rwanda, Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ,Abdelmadjid Tebboune Rais wa mpito wa Chad , Denis Sassou Nguesso wa  Jamhuri ya Kongo-Brazzaville, Mohamed Bazoum wa Niger,  Abdelmadjid Tebboune wa Algeria, Nana Akufo-Addo wa Ghana.

 

Habari Zifananazo

Back to top button