Aagiza mgomo daladala Mwanza usitishwe

MWANZA: MADEREVA wa usafiri wa umma ’daladala’ Mkoa wa Mwanza wametakiwa kuacha mgomo na kurejea barabarani ili waendelee kuhudumia umma.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi amesema wamekubaliana na uongozi wa madereva daladala wamalize mgomo.

‘’Tumekubaliana kwa pamoja magari yote yarudi barabarani ndani ya saa mbili tokea hivi sasa. Saa nane kamili madereva wote wanatakiwa kurejea barabarani’’ amesema.

Amesema kwa dereva yeyote atakaye kaidi agizo la serikali atawajibishwa.

‘’Tumewaelekeza polisi katika maeneo mbalimbali wasimamie suala la usalama katika,’’ ameagiza DC huyo.

Naye Mwenyekiti wa Wamiliki wa wasafirishaji Mkoa wa Mwanza, Yusuph Lupiliya amesema walipokea taarifa ya vipeperushi kuwa Machi 11,2024 kutakuwa na mgomo wa daladala ila hajui taarifa hiyo imetolewa na nani.

‘’Tulipata taarifa za mgomo tokea juzi lakini hatujui ni nani aliendika vipeperushi hivi na kusambaza. Madereva wetu wameweka mgomo huu bila taarifa sisi tuliwambia wasigomee kiukweli wenzetu wamekiuka.’’ Amesema Lupiliya.

Ameahidi wataongea na madereva wa daladala ambapo kwa sasa wamekusanyika katika ukumbi wa Gandi ili waweze kurejea makazini na kuendelea na kazi ifikapo saa nane mchana

Habari Zifananazo

Back to top button