MKUU wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu amewaagiza maofisa ugani, watendaji wa vijiji na viongozi wote wilayani humo, kuhakikisha ndani ya wiki moja wakulima wote wanaandikishwa katika daftari la wanufaika wa mbolea za ruzuku.
Buswelu ametoa agizo hilo Oktoba 21,2022, katika kikao cha ufunguzi wa msimu wa kilimo wilayani Tanganyika, kilichofanyika kikiwahusisha wadau mbalimbali wa kilimo.
“Malengo ni kuandisha zaidi ya wakulima 75,230 kwenye Wilaya yetu, leo tarehe 21, Oktoba tunao wakulima wachache sana,13,478. Hatuoni sababu ya kuendelea kuwa wachache, hii idadi ni ndogo sana,” amesema.
Mwakilishi wa Ofisa Kilimo na ushirika Wilaya ya Tanganyika, Jaliwa Ntibiyoboka, amesema katika maandalizi ya msimu wa kilimo 2022/23, Wilaya ya Tanganyika inatarajia kulima mazao ya chakula hekta 125,122 na matarajio ni kuzalisha tani 478,601, ambapo msimu wa 2021/22 Wilaya ilizalisha tani 436,131.
37 za mazao ya chakula.