Abiria mwingine afariki dunia ndani ya KQ

shirika la ndege la Kenya Airways

ABIRIA mwingine amefariki ndani ya ndege ya shirika la ndege la Kenya Airways ikiwa ni karibu wiki mbili tangu kisa kama hicho kuripotiwa na shirika hilo.

Kifo hicho kilithibitishwa siku ya Ijumaa na shirika la ndege katika taarifa.

“Baada ya uchunguzi zaidi, wahudumu wa afya waliokuwemo ndani ya ndege hiyo walithibitisha kuwa abiria huyo ameaga dunia,” ilisema taarifa hiyo.

Advertisement

Ndege hiyo ilikuwa ikielekea New York kutoka Nairobi. KQ ilisema abiria huyo ambaye jina lake halikutajwa aliaga dunia Septemba 2, 2022 mwendo wa 12.30 asubuhi. Kisa hicho kilitokea ndani ya ndege ya KQ002.

Abiria aliyefariki katika mojawapo ya ndege zake kutoka New York hadi Nairobi wiki iliyopita alikuwa raia wa nchi mbili Marekani na Kenya.

Mamlaka zilimtambua kama Peterson Njuguna Mwangi mwenye umri wa miaka 66 mkazi wa Lewisburg Pennsylvania.