Abiria stendi ya magufuli kupimwa TB

DAR ES SALAAM; SERIKALI imeweka mkakati wa kuwapima ugonjwa wa kifua kikuu (TB) wasafiri wanaoingia na kutoka katika mkoa huo kupitia stendi ya Magufuli.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Kifuu na Ukoma, Manispaa ya Ubungo, Catherine Saguti katika Mkutano wa mwaka wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma (NTLP).


“Manispaa ya Ubungo imeweka mkakati wa kutokomeza ugonjwa huo ifikapo 2030 kwa kushirikiana na Idara zote za serikali ikiwemo uvuvi, mifugo, ardhi na mipango miji ili kutekeleza jukumu hili,

“Manispaa ya Ubungo tuna Stendi kubwa ya Magufuli,inayopokea wageni wengi kutoka mikoa mbali mbali, hivyo kupitia gari tembelezi tunapima wagonjwa wote wanaoingia ili kubaini kama wana vimelea vya TB,”amesema.

Ameongeza  katika kuendeleza juhudi za kudhibiti ugonjwa huo Serikali imeboresha huduma za uchunguzi na uuguzi kwa kuwekeza katika teknolojia ya kisasa za mashine za Gene Xpert 50, Mashine za ECG 179 ambazo utumika kutambua vimelea vya TB kwa haraka na uhakika.

Naye, Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma jijini Dar es Salaam, Dokta Mbarouk Seif Khaleif amesema takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania watu 87 hupoteza maisha kila siku kutokana na ugonjwa huo na kuifanya kuwa miongoni mwa nchi 30 duniani zenye maambukizi makubwa ya TB.

Amesema Tanzania kila mwaka watu 137,000 huugua TB na husababisha vifo 32,000, sawa na vifo 87 kila siku kati ya vifo hivyo, 33 ni vya waliokuwa wanaishi na virusi vya ukimwi (WAVIU).

Akizungumza na HabariLeo, Dokta Mbarouk amesema TB ni janga ambalo linaua kimya kimya na hugharimu wastani wa asilimia 7 ya pato la taifa huku Dar es Salaam ikiwa kinara kwa asilimia 17.

Amesema, mkoa huo unapokea wagonjwa wengi kutoka mikoa mingine wanaofuata matibabu na mara wapimwapo, hubaini kuwa na maradhi ya TB na kufanya idadi hiyo ihesabike kama wao pia ni wakazi wa Dar es Salaam wakati sivyo hivyo.

Dk Mbarouk ametaja takwimu za miaka mitano za Kifua Kikuu kwa Mkoa wa Dar es Salaam mwaka na idadi kwenye mabano kuwa ni 2018 watu waliopata maambukizi ni (15481) 2019 (15,091), 2020 (13,217), 2021 (14,657) na 2022 ni watu (16,661

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button