MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood ameahidi kutengeneza madawati 400 kwa lengo la kupunguza uhaba unaozikabili shule za kata ya Mwembesongo na Kingolwira.
Abood ametoa ahadi hiyo kwenye ziara yake ya kusikiliza changamoto za wananchi katika kata hizo ikiwa na utekelezaji wa Ilani Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kulikiliza na kutatua kero cha wananchi.
Licha ya kutoa ahadi hiyo, akiwa kata ya Kingolwira alikabidhi shuka 30 kwa ajili ya matumizi ya wagonjwa wa Kituo cha Afya Kingolwira baada ya kupata taarifa ya uwepo wa upungufu mkubwa wa shuka.
Mbunge huyo alikabidhi shuka hizo kwa Diwani wa kata hiyo ,Madaraka Bidyanguze pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kituo cha Afya, Simba Waziri wakiwemo na viongozi wengine wa CCM.
Abood aliahidi kukarabati madirisha ya zamani 15 yenye nyavu na kuweka mapya ya vioo vya aluminium katika wodi ya wanawake na ya wanaume , ununuzi wa mashine ya kufuria shuka na mabenchi saba ya kukalia wagonjwa kwenye kituo hicho.
Kwa upande wa Vikundi vya Ujasiliamali, Mbunge huyo alikabidhi hundi ya milioni moja (sh 1000,000 ) kwa ajili ya kukuza mtaji wa wanawake Wajasiliamali wa Kikundi cha Umoja ni Ushindi wanaofanya biashara soko la Kingolwira .
“ Nimefika hapa pamoja na mambo mengine lakini niliwaahidi kuwapatia fedha za kuimalisha mtaji wa kikundi chenu na leo ninawakaabidhi hundi y a sh milioni moja ya kuendeleza biashara zetu hapa sokoni Kingolwira” alisema Abood
Kwa upande wao wanawake wa kikundi hicho kpitia kwa mwenyekiti wake , Fatuma Omary alimshukuru mbunge Abood kwa kuwawezesha fedha kwa ajili ya kuboresha mtaji wao ili kukundi chao kuweze kuwa na maendeleo makubwa .
“ Tunamshukuru mheshimiwa mbunge wetu kwa kutupatia mtaji wa Sh milioni moja , sisi wanachama wakikundi hiki ambao ni wanawake 40 , tutatumia mtaji huu kuuendeleza zaidi tuweze kuinuka kiuchumi na kuwasaidia watoto wetu “ alisema Fatuma.
Katika hatua nyingine Mbunge Abood aliwapatia samani za Ofisi ya Wanawake wa CCM Kata ya Kingolwira Meza, Viti na Vitu vingine vya kiofisi ili iweze kuwa hadhi zaidi.