Acheni tamaa- Rais Samia

RAIS Samia Suluhu Hassan  amewataka wafanyakazi wa NSSF kuweka tamaa pembeni kwa sababu kila kitu wanachokifanya Mungu anawaona.

Rais ametoa kauli hiyo leo Juni 14, 2023 alipotembelea mradi wa ujenzi wa Hoteli ya nyota tano itakayogharimu sh bilioni 93 hadi kukamilika kwake ambapo itasaidia kuimarisha sekta ya utalii na pia itaongeza tija katika mfuko kwa sababu itasaidia kutumisha mfuko huo

Advertisement

“Mungu atawalipa kila mtu kutokana na kile alichokifanya katika utumishi wako wa kuwatumikia Watanzania.”Amesema

Amesema, kutokuwa na tamaa kutasababisha mapato ya mfuko kukua na kuwa na manufaa mapana kwa wafanyakazi na kuwezesha mfuko kuendelea na ujenzi wa vitega uchumi vingi zaidi hali itakayoimarisha uchumi