Chama cha ACT Wazalendo kimetoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa aliyefariki jana wakati akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jana.
Katika taarifa yao ya pole waliyoitoa leo Februari 11, 2024, mwenyekiti wa chama hicho, Juma Duni Haji amemuelezea Lowassa kama kiongozi aliyewatumikia wananchi kwa moyo mkunjufu katika nafasi zake mbalimbali.
“Taifa litamkumbuka kwa mchango wake kwenye maendeleo ya nchi yetu, kwa niaba ya ACT Wazalendo na chama na kwa niaba yangu binafsi, natoa pole kwa mama Regina Lowassa na familia nzima ya hayati Lowassa,” imeeleza taarifa hiyo.
Aidha, mwenyetiki huyo ametuma salamu za rambirambi kwenda kwa Rais Samia Suluhu sambamba na kutoa pole kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.