ACT Wazalendo yasaka ufalme Afrika

CHAMA cha ACT Wazalendo kinatazamia ndani ya miaka mitano ijayo kuwa taasisi imara zaidi inayojiendesha kwa misingi ya kitaasisi kuliko vyama vyote vya siasa Afrika, Katibu Mkuu Ado Shaibu ameeleza.

Akizungumza leo Machi 8, 2024 na waandishi wa habari, Ado ambaye jana alichaguliwa kushika nafasi hiyo kwa mara nyingine, alisema lengo la chama hicho ni kuwa imara kimtandao kwa upande wa wanachama na uongozi.

“Jana nilieleza mbele ya Halmashauri Kuu kwamba kipaumbele cha kwanza, kitakuwa kuendeleza  kazi hii ya uimarishaji wa chama,”amesema Ado Shaibu.

Ado amesema kwa miaka minne aliyokuwa katika nafasi hiyo, wamefanikisha uchaguzi katika majimbo yote 214 ya Tanzania Bara na 50 ya Zanzibar na mkioa 39 ya kichama iliyopo Tanzania.

Habari Zifananazo

Back to top button