Adakwa akidai ni mshauri wa Rais Samia mambo ya kijeshi

POLISI Mkoa wa Tanga imefanikiwa kumkamata mkazi wa Dar es Salaam, Zainabu Kagoso (50), akidaiwa kujitambulisha kuwa ni mshauri wa Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika mambo ya kijeshi na kutumia njia hiyo kutapeli ofisi za serikali na maeneo mbalimbali wilayani Kilindi.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Henry Mwaibambe amesema kuwa mtu huyo mara baada ya kukamatwa alidai ni ofisa usalama yupo Tanga kwa kazi maalum, ambapo amekuja kufuatilia kazi mbalimbali alizotumwa.

“Tumemkamata mtu mmoja mwanamke mkazi wa Ukonga Dar es Salaam, amekuja mkoani Tanga hasa wilaya ya Kilindi, akiwa anaenda ofisi mbalimbali za serikali, akidai yeye ni ofisa usalama wa Taifa na amekuja kwa kazi maalum na kwamba yeye ni mshauri wa Rais Samia Suluhu Hassan katika mambo ya kijeshi, amekuja kuangalia kazi mbalimbali aliyotumwa, ” amesema Kamanda Mwaibambe.

Advertisement

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *