Adebayor astaafu soka

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Arsenal na Tottenham Hotspurs, Emmanuel Adebayor ametangaza kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 39.

Akiwa nchini England Adebayor alizichezea timu za Arsenal, Manchester City, Tottenham na Crystal Palace. Alifunga mabao 97 ya Premier League kwa muda wote wa Spurs, Arsenal na Man City wakati akiwa England.

Fowadi huyo alikuwa na wakati mzuri katika vilabu vyake vingine, alishinda tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka wa Afrika mnamo 2008 wakati akiwa Arsenal. Pia alitawazwa mwanasoka bora wa mwaka wa Togo kwa miaka mitano mfululizo kati ya 2005 na 2009.

Adebayor alikuwa kwenye basi la timu ya Togo ambalo lilivamiwa na magaidi mwaka wa 2010 wakati timu hiyo ikielekea Angola kwa ajili ya michuano AFCON. Watu watatu waliuawa na watu tisa kujeruhiwa katika shambulio hilo.

Adebayor alitumia muda mwingi wa miaka yake nchini Uingereza, lakini pia alifurahia maisha yake nchini Ufaransa akiwa na Metz na Monaco mwanzoni mwa maisha yake ya soka na aliwahi kuwa na miamba ya Hispania, Real Madrid mnamo 2011.

Mara ya mwisho mshambuliaji huyo alikuwa na timu ya Semasi ya nchini kwao Togo.

Habari Zifananazo

Back to top button