Ado Shaibu aipa neno CCM

PWANI: KATIBU Mkuu Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema kitendo cha chama cha ANC kushindwa kupata kura za kuunda serikali peke yake inapaswa kuwa funzo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Ado amesema hayo leo Juni 01, 2024 wakati akizungumza na viongozi wa chama hicho Mkoa wa Pwani katika kikao kilichofanyika Kata ya Mwandege Jimbo la Mkuranga.

“Kinachoendela kwa ANC nchini Afrika Kusini kinapaswa kuwa funzo kwa CCM kuwa ikipuuza hisia za wananchi nao watazungumza kupitia sanduku la kura,” amesema Ado.

Advertisement

Kwa mara ya kwanza tangu 1994 ANC imeshindwa kufikisha 50% ya kura ili kuunda serikali.

Aidha amesema kuwa Chama cha ACT Wazalendo kinapanga kuwasiliana na asasi za kiraia mbalimbali kufungua kwsi mahakamni kuhakikisha uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa unasimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi badala ya Tamisemi.