Adolph Mbinga afariki dunia

Marehemu Adolph Mbinga

MPIGA solo mahiri nchini Adolph Mbinga amefariki dunia.

Kwa mujibu wa mwanamuziki Mwinjuma Muumin aliyewahi kufanya kazi na na Mbinga katika bendi ya Mchinga Sound ‘Kipepeo’,  amesema alikutwa na mauti usiku wa kuamkia leo kijijini kwao Mpute , Wilaya ya Nachingwea.

“Nimepokea taarifa kutoka kwa kaka yake kwamba Mbinga alifariki jana usiku, ni msiba mkubwa kwa tasnia ya muziki wa dansi nchini,”amesema Muumin na kumuelezea marehemu Mbinga kama mtu aliyemsaidia kwa kiasi kikubwa katika masuala ya muziki nchini.

Advertisement

Mbinga atakumbukwa kwa umahiri wake katika gitaa la solo akiwa na bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ na albamu yao ya Kisa cha Mpemba, pia alikuwa kiongozi muasisi wa bendi ya Mchinga Sound na kushiriki katika albamu ya kwanza ya bendi hiyo iitwayo Kisiki cha Mpingo.

Baadhi ya nyimbo alizotunga wakati wa uhai wake na kushiriki kupiga gita la solo ni Neema wa bendi ya Diamond Sound, Kisa cha Mpemba bendi ya Twanga Pepeta’, Mdomo, Binadamu na Mto Wenye Mamba bendi ya Mchinga Sound.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *