Afande Sele apongeza wananchi kuhamia Msomera

“Ongezeko la watu ni ongezeko la mahitaji na ongezeko la mahitaji ni ongezeko la binadamu hivyo mnaohama kwa hiari niwapongeze kwani mnapokwenda mtapata mahitaji muhimu ya kibinadamu ikiwemo shughuli za uzalishaji mali”

Hayo ni maneno ya Balozi wa Uhifadhi wa Mazingira , Suleimani Msindi maarufu kwa jina la kisanii, Afande Sele ambaye anasema kuhama kwa wananchi kwenda Msomera ni jambo jema lenye mslahi mapana ya nchi ikiwemo uhifadhi

Pia ametoa rai kwa wananchi kujiandikisha kwa wingi ili waweze kuondoka katika maeno salama na bora ya kufanyia shughuli zao za kiuchumi

Advertisement

Katika kijiji cha Kayapus cha eneo la Kimba ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro ambapo Afande Sele alizungumza na wanahabari na kujionea hali halisi ya uoto wa asili kujirudia sanjari na wanyama kufika kwenye maeneo ya makazi na kuendelea kujitafutia malisho yao ya kila siku

“Endeleeni kuondoka katika maeneo ya uhifadhi kwani watu ni wengi mahitaji ni makubwa lakini mnapoenda maeneo mengine mnapata fursa za kimaendeleo”

Alisema mwaka 1959 watu walikuwa 8000 katika eneo hilo lakini kadri siku zikivyoenda idadi hiyo ya watu iliongezeka na kufika zaidi ya watu milioni 1 na hivi sasa katika kijiji hicho mifugo na watu wameendelea kupungua kutokana na kuhama kwa hiari kwenda Msomera.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *