Afrika imekuaje? Ronaldo aweka rekodi!

AFRIKA limekuwa Bara lenye bahati mbaya mwaka huu wa Kombe la Dunia, baada ya timu zote tano kushindwa kupata ushindi katika michezo ya ufunguzi, huku Ghana iliyokuwa timu ya mwisho ikizima ndoto hiyo baada ya kunyukwa mabao 3-2 na Ureno.

Senegal, Cameroon na Ghana wote wamepoteza michezo ya kwanza, Tunisia na Morocco walau wameambulia sare ya bila kufungana katika michezo yao.

Mchezo ulioisha hivi punde ni kati ya Ureno na Ghana, ambao ulikuwa wa kusisimua na kushuhudia Ghana wakianza vizuri, wakizuia kwa nidhamu kubwa na kushambulia kwa kushtukiza, ambapo mpaka mapumziko walienda bila ya kufungana.

Cristiano Ronaldo alifungua akaunti ya mabao kwa mkwaju wa penalty na dakika ya 65, dakika nane baadaye Andre Ayew alisawazisha. Ni kama walijisahau walinzi wa Ghana walipopandisha timu kufanya mashambulizi na Ureno kufanya Kaunta iliyowapa bao la pili lililofungwa na Joao Felix dakika ya 78.

Ghana waliendelea kucheza mchezo wa kutanua uwanja huku wakitafuta bao la kusawazisha bahati mbaya ikawakuta na kufungwa bao la tatu kupitita Rafael Leao dakika ya 80.

Dakika ya 89 Osman Bukari akaipatia Ghana bao la pili hata hivyo juhudi za waghana ziliishia hapo na mchezo kuisha kwa mabao 3-2 Ureno wakipata ushindi.

Rekodi iliyowekwa katika mchezo huo, Cristiano Ronaldo amekuwa binadamu wa kwanza kufunga Kombe la Dunia mara tano, yani mwaka 2006, 2010, 2014, 2018, na 2022. Kwa miaka hiyo sasa Ronaldo amefikisha mabao manane.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x