Afungwa Maisha kwa ubakaji

MKAZI wa Mtaa wa Kiranyi kata ya Sakina Jijini Arusha ,James Juma{28} amefungwa kifungo cha maisha kwa kosa la kubaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 11.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mwandamizi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha,Herieth Marando baada ya kuandikwa na Hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha aliyesikiliza Kesi hiyo ,Pamela Meena.

Hukumu hiyo imesema kuwa Juma alitenda kosa hilo Septemba mwaka jana baada ya kumteka na kumtishia kwa kisu mtoto huyo akitokea shule na kumpakia katika usafiri wa bodaboda hadi nyumbani kwa mtuhumiwa na kumbaka bila ridhaa yake hatua ambayo ilimpa maumivu makali Mtoto huyo.

Hukumu ya Meela ilieleza kuwa katika usikilizwaji wa kesi hiyo upande wa Jamhuri ulikuwa na mashahidi watatu na upande wa utetezi ulikuwa na mashahidi wawili.

Katika usikilizwaji wa kesi hiyo Mahakama iliridhika na ushahidi wa mashahidi wote uliotolewa na upande wa Jamhuri na kujiridhisha pasipo shaka kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo.

Hakimu Meela katika hukumu yake amesema Mahakama imeona na imeridhika kuwa kitendo kilifanyika kwa mtuhumiwa kutenda kosa hilo kwa kumteka na kumtishia kwa kisu na baadae kumpeleka nyumbani na kumbaka.

Mahakama iliona maelezo ya mtuhumiwa ya Novemba 28 mwaka jana yaliyoeleza mtuhumiwa alikiri kosa hilo na utetezi wa mashahidi Mahakamani haukuwa na nguvu au hakuwa na hoja za kupinga maelezo yake ya awali aliyoyatoa polisi wakati anahojiwa.

Hakimu Meela alisema kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo mapema Septemba mwaka jana na mzazi wa kike aligundua mtoto wake kufanyiwa unyama huo na kumpeleka polisi na kupatiwa PF3 na kwenda hospital kupatiwa matibabu.

Baada ya maelezo ya mashahidi Mahakama imeridhika na ushahidi wa mashahidi wa Jamhuri na kutupilia mbali ushahidi wa utetezi kwa madai kuwa haukuonyesha au haukueleza bayana kama mtuhumiwa hakutenda kosa hilo siku hiyo.

Kufuatia hali hiyo,Hakimu Meela alimtia hatiani Mtuhumiwa na alipopewa nafasi ya kujitetwa mtuhumiwa alishikwa na kigugumizi baada ya kupewa nafasi hiyo na badala yake alikaa kimya muda wote.

Baada ya kuonyesha hali hiyo Hakimu alimpa nafasi Mwendesha Mashitaka wa Serikali,Grace Medikenya kama anachakuzungumza na alidai hana Cha ziada  na Hakimu alitoa hukumu ya kifungo cha maisha kwa mtuhumiwa.

Baada ya kuhukumiwa Maisha,Hakimu Marando alimweleza Juma kama hajaridhika na hukumu anaweza kukataa rufaa Mahakama ya juu kupinga hukumu hiyo na nakala ya hukumu itakuwa tayari baada ya wiki mbili.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x