Ahimiza kuwapa ushirikiano makarani

MKUU wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amewaasa wananchi wa mkoa huo, waendelee kutoa ushirikiano kwa makarani wa sensa ya watu na makazi.

Mongella alisema hayo jumatano baada ya kukagua maendeleo ya sensa katika jamii ya wawindaji wa kabila la Wahadzabe wilayani Karatu.

Alisema jamii hiyo wameitikia mwito wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kuhesabiwa na wametoa ushirikiano kwa makarani wa sensa.

Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Dadi Kolimba alisema katika wilaya hiyo walianza kuhesabu watu usiku wa kuamkia Agosti 23 katika hoteli na kambi za wavuvi.

Kolimba alisema sensa inaenda vizuri na wataendelea kuisimamia kwa umakini zaidi hadi itakapokamilika. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu, Karia Rajabu alisema jamii ya Wahadzabe walioko katika kambi ya Kijiji cha Qangdend na Kijiji cha Engamaghan tayari kaya 50 zimehesabiwa.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Engamaghan, Idhaya Thume alimshukuru Rais Samia kwa kuwapa nyama ambayo ni chakula chao kikuu na hiyo ikasaidia wao kuhesabiwa kwa urahisi kwa kuwa hawakwe

Habari Zifananazo

Back to top button