Ahly wameingia ubaridi bwana!

DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa timu ya Al Ahly SC ya Misri, Marcel Koller, amesema mchezo wa Robo Fainali wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba kesho utakuwa mgumu kwa kuwa wapinzani wao ni wazuri na wana uzoefu wa kutosha.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Koller amesema mara zote wanapokutana na Simba huwa wanawapa mchezo mgumu.

“Tumejiandaa kila tuwezalo. Sisi ni mabingwa watetezi hivyo ni lazima tupambane ili kupata ushindi mzuri kesho na kutengeneza mazingira rafiki ya kutetea taji letu,” amesema Koller.

pharmacy

Akizungumzia michezo miwili ya hivi karibuni Koller amesema: “Tumecheza na Simba katika michezo miwili ya hivi karibuni ya AFL na ilikuwa michezo migumu yenye matokeo ya sare, hivyo kwetu sisi na wao ni sawa kwa kuwa ni timu shindani kwetu,” amesema.

Alipoulizwa kuhusu pengo watakalolipata kuwakosa wachezaji muhimu kikosini Imam Ashour, Aliou Dieng na El Shanawy, Kocha huyo amesema wana wachezaji wengi kwenye kila nafasi, kuwakosa wachezaji kadhaa hilo sio jambo linalowaumiza kichwa.

“Ninaamini wachezaji waliopo na wanatosha kupambana hapo kesho,” amesema Koller.

Naye, mlinzi wa Al Ahly, Ramy Rabia amesema wapo tayari kuwakabili Simba hapo kesho

“Tunacheza kitimu, tutaenda uwanjani hapo kesho tukiwa na utimamu wa akili na mwili kuhakikisha tunatekeleza majukumu yetu kwa namna kocha atakavyotutaka,” amesema Ramy

Habari Zifananazo

Back to top button