HIFADHI ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Maingilio ya Mto Ruvuma (Marine Park) iliyopo kijiji cha Msimbati Halmashauri ya Wiliaya ya Mtwara imegundua aina tano za kasa ambao wataenda kuongeza utalii.
Akizungumza wiki hii mkoani mtwara katika uzinduzi wa mradi wa uhifadhi wa kasa, mhifadhi bahari wa hifadhi hiyo , Mustapha Issa amesema elimu waliyotoa itasaidia kuongeza hamasa na juu ya uhumimu wa kiumbe huyo.
Utoaji elimu ya hamasa kwa wananchi umehusisha maeneo matano ya halmashauri hiyo ikiwemo Msimbati, Ruvula, Litembe, Kingumi, Litokoto.
Amesema hali itayopelekea kiumbe huyo kutoweka ni kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu wakiachana na athari ya mabadiliko ya hali ya hewa na uchafuzi, kiumbe huyo amekuwa adimu kwa kipindi hiki hasa katika maeneo yao kutokana na kuvunwa kwa ujangili, shughuli za kimaendeleo kama vile uharibifu wa fukwe zimechangia mazalia ya kiumbe huyo kupotea kabisa.
Adha, amezitaja aina hizo tano za kasa zilizopo kwenye hifadhi hiyo ikiwemo kasa wa Kawaida, Ng’amba hao hutumia sehemu hiyo ya hifadhi kama sehemu ya malisho pamoja na mazalia wengine ni noa, duvi na likome ambao hutumia sehemu hiyo kwa ajili ya malisho tu ila mazalia yake yako sehemu zingine duniani.
Mradi huo unafadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali nchini la Wentworth linalojihusisha na shughuli za uchimbaji wa gesi asilia mkoani humo ambapo mwakilishi wa shirika hilo Neema Ndikumwami amesema shirika linatambua umuhimu wa kuhusika,kujihusisha kwenye miradi ya kuhifadhi viumbe vya bahari.
Mradi huo ni wa mwaka mmoja ambao unaanza rasmi Agosti 2023 mpaka Julai 2024 na ni mradi wa pili kwa shirika hilo kushiriana na hifadhi hiyo na serikali ya kijiji hicho kwani awali walipanda miti zaidi ya 20,000 aina ya mikoko kwenye eneo hilo huku akitoa wito kwa jamii hiyo kushirikiana na hifadhi kwa kuona umuhimu wa kuhifadhi na kuokoa viumbe hivyo, uzinduzi ambao umeenda sambamba na kauli mbiu inayosema ‘Okoa Kasa Wapo Hatarini Kutoweka’.
Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara ambaye pia ni Ofisa Maliasili mkoani humo, Ronald Panga amesema kwa kuwa mradi huo upo kwa wananchi wa maeneo hayo basi elimu hiyo ya uhifadhi wa kasa iwe endelevu kwa viijiji vyote vilivyopo mpakani mwa bahari hiyo huku akiwataka wafadhili hao kuangalia namna ya kuweza kuwafikia wananchi waishio maeneo hayo lakini pia taasisi zote ikiwemo sekta ya elimu (Mashuleni) ili wakawe mabolozi wazuri wa kuhakikisha viumbe hivyo vinahifadhiwa.
Mkazi wa kijiji cha Msimbati kwenye halmashauri hiyo, Juma Waziri ameseme, ‘’Nimepokea kwa furaha sana mradi huu na tunawashukuru sana viongozi wetu kwa kutuletea mradi huu kwasabau unaenda kuimarisha utunzaji wa viumbe hivi adimu na sisi kama wananchi wa maeneo haya yanayozunguka mradi tunaahidi kutoa ushirikiana nzuri tu katika suala hili la uhifadhi kwasababu faida yake ni kubwa hasa utalii na uchumi utaotokana na viumbe hivi.” amesema.
Comments are closed.