Ajali barabarani zaua watu 382 miezi mitatu

BUNGE limeelezwa kuwa ajali za barabarani zimeua watu 382 kati ya Oktoba hadi Desemba mwaka jana.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Vita Kawawa alisema idadi hiyo ni sawa na ongezeko la watu 15 sawa na asilimia 4.1 ya watu 367 waliokufa kwa kipindi kama hicho mwaka 2021.

Vita amebainisha hayo bungeni Dodoma jana wakati akiwasilisha taarifa ya mwaka ya shughuli za kamati kwa kipindi cha Februari mwaka jana hadi Januari mwaka huu.

Aliwaeleza wabunge kuwa kati ya Oktoba hadi Desemba mwaka jana matukio ya ajali yaliyosababisha vifo ni 281.

Vita alisema idadi hiyo ni sawa na ongezeko la matukio manane ambayo ni sawa na asilimia 2.9 ya matukio 273 yaliyoripotiwa kipindi kama hicho mwaka 2021.

Alisema uchambuzi uliofanywa na kamati hiyo ulionesha kuwa ajali za barabarani zimekuwa zikichangiwa na baadhi ya askari wa usalama barabarani kujihusisha na rushwa na hivyo kutotimiza wajibu wao kushughulikia makosa ya barabarani.

Alitaja sababu nyingine ni uhaba wa vitendea kazi yakiwamo magari ya doria katika barabara kuu, taa za kuongozea magari, upungufu wa taa za kupima mwendokasi wa magari, upungufu wa kamera na vipima ulevi.

Vita alitaja sababu nyingine ni kukosekana kwa utashi wa kisiasa kwa baadhi ya wanasiasa na hivyo kuingilia utekelezaji wa sheria za usalama barabarani.

“Mathalani, kuwazuia askari kuwakamata bodaboda au bajaji wanapofanya uvunjifu wa sheria,” alisema Vita.

Wabunge walielezwa kuwa vyanzo vingine vya ajali ni ubovu wa baadhi ya barabara, na hulka za kibinadamu kuamini kuwa ajali hazizuiliki na hivyo kuendesha pasipo kuzingatia sheria ya usalama barabarani.

Vita alitaja chanzo kingine ni madereva wengi wasio na sifa ya udereva.

“Hali hii inasababishwa na mfumo uliopo wa utoaji leseni za udereva kutoa mwanya kwa watu wasio na sifa ya kuwa dereva kupata leseni,” alisema Vita.

Aliongeza: “Aidha, kamati ilibaini kuwa katika siku za karibuni kumeibuka wimbi la magari ya watu/taasisi binafsi na za umma, kufungwa ving’ora kinyume na utaratibu ilihali wakiwa hawana uelewa wa kutosha kuhusu matumizi ya magari yenye ving’ora

Habari Zifananazo

Back to top button