Ajali: Mashabiki wanne Namungo wapoteza maisha

UONGOZI wa Namungo FC umetoa taarifa kuwa gari la mashabiki wake lililokuwa linatoka Lindi kwenda Dar es salaam kuishangilia timu hiyo katika mchezo dhidi ya Yanga limepata ajali na mashabiki wanne kupoteza maisha.

Katika taarifa hiyo imeeleza kuwa watu 16 wamejeruhiwa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mashabiki hao waliokuwa wanatoka Lindi ili kuwahi mchezo huo leo saa 1:00 usiku katika uwanja wa Azam Complex.

Advertisement

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Miteja karibu na Somanga. “Kwa sasa majeruhi wamepelekwa katika kituo cha afya Tingi Wilaya ya Kilwa Mkoa wa Lindi,” imeeleza taarifa hiyo.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *