Ajali mbaya Arusha

Watu 15 wapoteza maisha

ARUSHA: Watu 15 wamefariki dunia papo hapo mkoani Arusha katika ajali ya barabarani iliyohusisha magari matatu.

Akiwa katika eneo la Kibaoni Ngaramtoni ilikotokea ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha SACP Justine Masejo akizungumza amesema ajali hiyo imetokea leo Feb 24 majira ya saa 11 jioni baada ya lori lililokuwa likitokea Namanga kuelekea Arusha kuyagonga magari matatu.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha SACP Justine Masejo

Amesema  dereva aliyekuwa akiendesha lori hilo (jina kapuni)  alipoteza uelekeo hali iliyopelekea kuyagonga magari hayo.

Kwa mujibu wa Kamanda Masejo majeruhi wa ajali hiyo wapo katika hali mbaya na wanaendelea na matibabu.

Hata hivyo amewaomba wananchi ambao ndugu zao walikuwa wakisafiri kupitia barabara hiyo kufika katika hospitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru kwa ajili ya utambuzi wa marehemu pamoja na majeruhi ambao wanatibiwa hapo.

Habari Zifananazo

Back to top button