AJALI: Sita wapoteza maisha nchini Kenya

WATU sita akiwemo mtoto mdogo wamepoteza maisha katika ajili iliyohusisha magari matatu yakiwemo trekta na Isuzu katika eneo la Maili Tisa barabara ya Eldoret-Turbo nchini Kenya.

Kamanda wa Polisi wa Uasin Gishu, Ayub Gitonga alisema kuwa ajali hiyo ilihusisha abiria 14 waliokuwa kwenye magari hayo likiwemo Isuzu inayomilikiwa na Mamlaka ya Barabara nchini Kenya.

Mashahidi wanaeleza kuwa ajali hiyo iliyotokea jioni ya Jumatano, Novemba 23, 2022, ilitokea baada ya dereva wa trekta ambayo inasemekana haikuwa na taa kujaribu kuingia barabara kuu kulipokuwa na magari mengine ambayo pia yalikuwa kasi.

Majeruhi walikimbizwa katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi kwa matibabu (MTRH) huku miili ya marehemu ikipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha kituo hicho.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x