Ajali ya basi, gari ya msiba yaua watano

WATU watano wamefariki dunia  wengine   26 kujeruhiwa baada ya gari aina ya Toyota Coaster iliyokuwa ikisafirisha maiti kugongana uso kwa uso na Basi la Kampuni ya Kyela Express, wakati gari hizo mbili zilipotaka kulipita lori wilayani Rungwe, mkoani Mbeya.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Dk Vicent Anney, ajali hiyo imetokea leo Oktoba 11, 2022 majira ya asubuhi katika   kitongoji cha Kanyegere, Kijiji cha Ibula,  Kata ya Kiwira, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.

Dk Anney alipozungumza na Habarileo kwa njia ya simu, alisema miongoni mwa watu waliopoteza maisha ni pamoja na dereva wa Coaster iliyokuwa ikisafirisha maiti kutoka Dodoma, kwenda Kyela.

 

Habari Zifananazo

Back to top button