Ajali ya basi yaua 14 Lindi

LINDI: WATU 14 wamefariki dunia leo Novemba 26, 2023 katika ajali ya barabarani iliyohusisha basi la Kampuni ya Baraka lililokuwa likitokea Tandahimba, mkoani Mtwara kuelekea Dar es Salaam.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa moja asubuhi katika eneo la Mtama na chanzo cha ajali hiyo kikielezwa kuwa ni breki za basi hilo kufeli.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, John Imori amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Nyangao pamoja na majeruhi 26 wanaendelea na matibabu.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button