ZAIDI ya watu 13 wamepoteza maisha na wengine wawili wamejeruhiwa vibaya kufuatia gari walilokuwa wanasafiria kupoteza mwelekeo na kutumbukia mtoni.
Mkuu wa wilaya ya Songea, Wilman Ndile amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo alieleza kuwa gari hiyo aina ya Fuso iliwabeba wafanyabiashara waliokuwa wanatoka mnadani Kijiji Cha Ndongosi kuelekea Kijiji Cha Namatuhi wilayani humo.
Alisema,ajali hiyo ilitokea usiku wa saa 2;30, ambapo marehemu na majeruhi ni wakazi wa Manispaa ya Songea na maiti zimehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Songea.
“Tumepokea miili 13 wa ajali hiyo mnamo saa 9.
45 alfajiri, wanaume 7 na wanawake 6.
Umri wao ni kati ya miaka 28 hadi 50 hivi. Wametambuliwa na wafanyabiashara wenzao kwa majina na maeneo walipokuwa wanaishi.
“Miili yote 13 imehifadhiwa ktk chumba cha kuhifadhia maiti, hapa Songea,” amesema na kuongeza kuwa majeruhi wapo Kituo cha Afya Namanditi wakiendelea na matibabu.