WATU wawili wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa, baada ya gari aina ya Toyota Hiace kuligonga lori kwa nyuma katika eneo la Kwedizinga wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Sofia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo leo saa 12 asubuhi, wakati Hiace ilikuwa ikijaribu kupita lori, eneo ambalo alama haziruhusu kupita, hali ambayo dereva alishindwa na kuligonga lori hilo.
“Dereva huyo aliwapita polisi akiwa na mwendo wa kawaida, ila mbele kumbe aliongeza mwendo na kusababisha kutokea ajali wakiwa wanapanda mlima uliopo eneo hilo, ambalo kuna kona kali,” amesema Kamanda Jongo.