Ajali ya pikipiki yaua wawili Mtwara

MTWARA: WATU wawili wamekufa baada ya pikipiki waliyokuwa wakisafiria kuacha njia na kuanguka.

 

Akitoa taarifa hiyo leo kwa waandishi wa habari, Kamishna Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Mtwara (ACP), Nicodemus Katembo amesema ajali hiyo imetokea Disemba 17, mwaka huu majira ya saa 1:00 asubuhi.

Advertisement

 

Akitoa taarifa hiyo leo Disemba 18, 2023  Kamanda huyo amesema ajali imetokea eneo la Mlima kinombedo uliopo Kijiji cha mkwiti Barabara ya Newala-Mtama Wilaya ya Tandahimba mkoani humo.

 

Pikipiki hiyo yenye namba za usajili MC 828 BUT aina ya Sanlg iliyokuwa ikiendeshwa na Ismail Haili (65) mkazi wa kitangari wilayani Newala akiwa amempakia abiria Aisha Bakari (55) mkazi wa Kijiji cha mchewa  wilayani humo.

 

“Pikipiki hiyo iliacha njia na kugonga gema upande wa kushoto mwa barabara na kusababisha vifo papo hapo kwa mwendesha pikipiki huyo pamoja na abiria wake ambaye ni mkewe,” amesema Katembo

 

Miili ya marehemu hao imefanyiwa uchunguzi wa kitabibu katika hospitali ya nyangao iliyopo mkoani Lindi na baadaye kukabidhiwa ndugu  kwa mazishi.

 

“Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa mwendesha pikipiki kushindwa kuimudu pikipiki hivyo kuacha njia na kugonga gema.” Amesema ACP Katembo.

 

Aidha ametoa rai kwa madereva wa vyombo vya moto kwa ujumla kuzingatia sheria za usalama barabarani lakini pia wapanda pikipiki wazingatie kuvaa kofia ngumu/helmenti ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.

2 comments

Comments are closed.