WATU 12 wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa baada ya treni mbili kugongana nchini Ugiriki.
–
Tukio hilo lilitokea jana jioni nje ya Jiji la Larissa wakati treni hilo likitokea mji wa Athens kwenda Kaskazini mwa jiji la Thessaloniki na kugongana na treni nyingine ya mizigo.
–
“Tulisikia kishindo kikubwa kwa takribani sekunde kumi,” alisema Stergios Minenis, abiria ambaye aliruka baada ya ajali kutokea.”
–
Gavana wa eneo la Thessaly Konstantinos Agorastos aliiambia SKAI TV kwamba mabehewa manne ya kwanza ya treni ya abiria yalikatika katika ajali hiyo, na mabehewa mawili ya kwanza yalishika moto.
–
Imeelezwa abiria wapatao 250 walio na majeraha madogo wamehamishwa salama kwa basi kwenda Thesaloniki.