Ajali yajeruhi tisa Arusha

WATU tisa wamejiruhiwa mkoani Arusha baada ya kutokea ajali iliyohusisha magari matatu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP, Justine Masejo amesema ajali hiyo imehusisha lori namba T.

673 AXB aina ya Scania, likiwa na tela namba T.464 AWZ,  likiwa na shehena ya mahindi likitokea Arusha kwenda Namanga liliyagonga magari mengine madogo.

Amesema majeruhi wanapatiwa matibabu katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru.

Habari Zifananazo

Back to top button