Ajali za bodaboda bado tishio

DAR ES SALAAM :Taasisi ya Tiba na Mifupa (MOI), inapokea wagonjwa takribani 700 kwa mwezi huku asilimia 60 ya wagonjwa hao wakitokana na ajali za bodaboda

Hayo yamesemwa  leo Julai 2,2024 na Dk Lemeri Mchome Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Tiba na Mifupa (MOI), wakati akipokea msaada wa vifaa mbalimbali kutoka kampuni ya WATU.

Advertisement

Ameshauri madereva wa pikipiki za abiria maarufu kama bodaboda na bajaji wabadili tabia zao wakiwa barabarani na kufuata sheria.

Isome pia:https://habarileo.co.tz/ajali-za-bodaboda-wanaumia-mifupa-ubongo/

Kwa upande Meneja Mkuu Msaidizi, Kampuni ya WATU,  Seuri Kuoko, amesema wametoa msaada huo unaolenga kuwasaidia wagonjwa hao ili waweze kurudi katika hali yao.

Naye Jumaa Almasi Meneja Ustawi wa Jamii lishe kutoka Taasisi ya MOI, amesema kumekuwa na baadhi ya wagonjwa wanaletwa hawana uwezo, hivyo msaada huo utasaidia kuwapatia matibabu. Vifaa vilivyokabidhiwa ni vifaa tiba, viti mwendo viwili na taasisi hiyo itagharamia matibabu wagonjwa 15.