Ajinyonga baada ya kukatazwa kwenda kwa mwenza

MKAZI wa Mtaa wa Nyihogo wilayani Kahama mkoani Shinyanga Mariamu Robert Ngasa (28) amefariki dunia kwa kujinyonga kwa kamba baada ya kugombezwa na baba yake mzazi kwa kosa la kutoroka nyumbani kwenda kwa mpenzi wake na kukaa wiki moja.

Kwa mujibu wa mama mlezi wa Mariamu Wiliam alisema kuwa binti alikwenda eneo la Mwime lenye wachimbaji wadogo kuuza vitumbua vinavyochomwa nyumbani hivyo tangu siku hiyo hakurejea nyumbani hali iyozua wasiwasi na kuanza kumtafuta bila mafaniko.

Baada ya siku saba alirejea mwenyewe nyumbani akiwana na fedha za mauzo kisha akafokewa na baba yake na kueleza alikutana na mpenzi wake aliyepata naye mtoto wa kwanza na ndiye aliyemrubuni kwenda naye nyumbani kwake kwa kipindi chote ambacho walikuwa wakimtafuta.

“Binti yangu alizalia nyumbani mtoto wake wakwanza kitendo ambacho sisi kama wazazi kilituumiza ,kwani hata huyo mwanaume aliyemzalisha hakuwahi kufika nyumbani ili kumtambua,hivyo baba yake aliingiwa na wasiwasi huenda akapata mimba nyingine kwa sababu alianza mahusiano na mpenzi wake hivyo aligombezwa na hakupigwa.”aliongeza

Aliendelea kusema baada ya kula chakula cha mchana marehemu alikula kidogo kwa sababu alikuwa na hasira na kuomba aende akapumzike,kwa sababu yeye ni mfanyabiashara wa mbogamboga alitokea mteja akihitaji huduma hiyo ikamlazimu kwenda ndani kuchukua na kukuta mlango wa chumbani anakohifadhia umefungwa kwa ndani, na kutumia nguvu kuufungua na kumkuta amejinyoka kwa kutumia kitenge cha nguo.

Akielezea baba mzazi wa Mariamu, Rahel William alisema kuwa Januari 18, 2024 alimhoji mwanae na kisha kukiri kwenda kwa mpenzi wake ambaye hakumtaja jina na kuishi nae kwa muda wa wiki moja ,ambaye alimwagiza kutoa taarifa kwa wazazi wake kuwa mwezi Febuari mwaka huu angekuja kujitambulisha na kisha akamuonya asirudie kutoroka nyumbani bila taarifa.

“Nilimgombeza tu na siku mpiga kwa sababu aliomba radhi na kusema mpenzi wake angekuja kwangu mwezi wa Pili hivyo mimi sikuwa na wasiwasi, kisha mimi nikaenda kazini baada ya muda nikapewa taarifa za kujinyonga kwa mwanangu.”alisema William

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema chanzo chake ni kugombezwa na baba yake mzazi baada ya kutoroka nyumbani.

“Mtoto akikosea lazima agombezwe,niwaombe wazazi tuwemakini katika malezi, watoto wengi wamekuwa na viburi,hawatiki kuelezwa makosa yao,Viongozi wa dini, kimila, walimu tushiriane katika kulea.

Habari Zifananazo

Back to top button