Ajinyonga wivu wa mapenzi

MKAZI wa kijiji cha majengo kata ya Ziwani Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara amekufa baada ya kujinyonga na mtandio kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Akizungumza leo mkoani Mtwara, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara ACP Mtaki Kurwijila amesema tukio hilo limetokea Februari 18, 2024 saa 12 asubuhi.

Amemtaja marehemu huyo kuwa ni Bakari Mtepa (65) ambaye alitoweka nyumbani kwake Februari 12, mwaka huu na kwenda kusikojulikana baada ya kutoelewana baina yake na mke wake.

‘’Mwili wa marehemu ulikutwa umefungwa na mtandio shingoni ukiwa umening’inia kwenye tawi la mkorosho,”

“Sababu za kujinyonga inasadikiwa kuwa ni wivu wa mapenzi, baada ya kumtuhumu mke wake kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mwenaume mwingine’’amesema Kurwijila”.

‘Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata katika eneo la tukio kuna karatasi iliyokuwa imeandikwa ikielezea sababu hizo  alizochokuwa marehemu kujinyonga”

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Lingula mkoani humo kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu.

Katika hatua nyingine mkazi wa kijiji na kata ya Makote wilayani Newala mkoani humo, Zamira Mohamed (20) amekunywa sumu ya panya aina ya rotax. Pia kujikata na wembe kwenye mguu wake wa kulia kwa lengo la kutaka kujiua.

Mwanamke huyo ana mtoto wa mwaka mmoja na miezi mitano, alifanya mamuzi hayo baada ya kulazimishwa kuolewa na mtu ambaye hamtaki.

Baada ya tukio hilo alipoteza fahamu kisha kufikishwa katika hospitali ya wilaya hiyo ambapo mpaka sasa anaendelea kupatiwa matibabu.

Amesema upelelezi wa tukio hilo ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mbele ya sheria.

Habari Zifananazo

Back to top button