Ajira mpya kupata mafunzo ya utumishi wa umma

  1. WAZIRI wa nchi Ofisi ya Raisi Menejimenti ya  Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama amewataka waajiri nchini kutumia Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kuendesha mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya nchini.

Mhagama ametoa agizo hilo katika mahafali ya 36 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika kampasi ya Mtwara huku akimuagiza Katibu Mkuu wizara ya Utumishi kufuatilia na kumpa taarifa ya utekelezaji wa mafunzo kwa watumishi wapya.

“Nitoe wito kwa waajiri wote hasa ambao waraka wake utumishi uliwaelekeza kukitumia chuo hiki kuendesha mafunzo ya waajiri kufanya hivyo,” amesema.

Advertisement

Aidha, Mkuu wa Chuo hicho (TPSC) Dkt Emmanuel Shindika  amesema idadi ya waajiri wanaotumia chuo hicho cha Utumishi kuendesha mafunzo elekezi kwa waajiriwa hairidhishi huku akiomba serikali kuwasisitiza waajiri kukitumia chuo hicho kutoa mafunzo kwa watumishi wapya kikamilifu.

“Idadi ya mwitikio wa waajiri kwenye taasisi, wizara na wakala za serikali kukitumia chuo cha Utumishi wa Umma kuendesha mafunzo elekezi ya awali Kwa watumishi wapya ni ndogo, ” amesema.

Katika mahafali hayo, jumla ya wahitimu 6,315 kutoka kampasi sita (Dar es Salaam, Tabora, Mtwara, Mbeya, Singida na Tanga) wametunukiwa vyeti baada ya kuhitimu masomo katika ngazi mbalimbali.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *