Ajira, uzalishaji kwa wakulima kuongezeka

DODOMA: SERIKALI imesema Itifaki ya Biashara ya Huduma ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ya mwaka, 2012 itatoa fursa na manufaa kwa nchi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji leo alipokuwa akiwasilisha bungeni maelezo kuhusu Azimio la Kuridhia Itifaki ya Biashara ya Huduma ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ya mwaka, 2012 (SADC Protocol on Trade in Services, 2012).

Ametaja baadhi ya manufaa hayo kuwa ni kuongezeka kwa uzalishaji kwa wakulima, ajira na thamani ya mazao ya kilimo kupitia kuimarika kwa huduma wezeshi za malipo, usafirishaji na mawasiliano.

“Kupatikana kwa soko kubwa la bidhaa na huduma lenye idadi ya watu takribani milioni 360 katika Jumuiya ya SADC.

“Kuongezeka kwa tija na ubora kwa bidhaa na huduma za Tanzania kutokana na kuongezeka kwa ushindani na hivyo kupelekea kupungua kwa gharama za kupata huduma.

“Upatikanaji wa bidhaa za huduma za aina mbalimbali nchini, uhawilishaji wa teknolojia kutoka nje ya nchi (technology transfer) kutokana na uwekezaji utakaofanyika nchini,” amesema Waziri Kijaji.

Habari Zifananazo

Back to top button